Wednesday, 27 April 2016

star of jerusalem clinic inapatikana wapi?

maeneo ya star of jerusalem clinic

Dar  es salaam

Mwanza

Arusha

Shinyanga

Musoma

Bukoba

Karagwe

Muleba

Kyelwa ;nkwenda

Geita

Katoro

Sengerema

Ukelewe

 

Tuesday, 19 April 2016

SIRI YA MATUNDA KATIKA MAISHA YA BINADAMU

Hapa nimeweka baadhi ya ya matunda ambayo ni muhimu kwenye maisha ya bina damu yoyote ili mradi bado huu mzima usikose kula tunda hata moja kwa siku ni mimi mtaalamu wako 
Tabibu S.LUHAMBA
TIBA YA MIMEA,MATUNDA NA VIUNGO

Monday, 18 April 2016

VIPINDIU VYA AFYA RADIONI

Sikiliza Vipindi vya Afya kila siku katika Radio Sengerema kwa wale waliopo Sengerema na Kila Radio iliyopo mkoani kwako

ANGALIA MOYO UNAVYO FANYA KAZI KAMA HAUNA MAFUTA

EPUKA ULAJI WA VYAKULA VYENYE MAFUTA MOYO UWE SAFI

HEART ATTACK

MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI IPASAVYO

MAGONJWA ya Moyo (Cardiovascular Diseases), ni miongoni mwa magonjwa yaliyoko kwenye kundi la ugonjwa usioambukiza. Haya ni magonjwa yale yote yanayoathiri moyo na mishipa yake. Kwa hiyo, magonjwa ya moyo yanajumuisha ugonjwa wa Kupanda kwa Shinikizo la Damu (High Blood Pressure/Hypertension). Hili ni tatizo sugu la kiafya linalohusisha kuongezeka kwa mgandamizo wa msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu.
Magonjwa mengine ni Koronari za Moyo (Coronary Heart Diseases). Huu ni ugonjwa wa moyo ambapo mafuta yanaganda ndani ya ateri koronari na kuziba kwa kiasi fulani au kuziba kabisa kwa ateri ya koronari ya/za moyo, hivyo kusababisha upungufu wa damu katika sehemu ya moyo ambayo hupata damu kupitia mishipa hiyo.
Ugonjwa huu wa Koronari za Moyo hudhoofisha misuli ya moyo kiasi cha kusababisha moyo kushindwa kusukuma kiwango cha kutosha cha damu (Heart Failure). Aidha, ugonjwa huu  husababisha Arithmia (Arrhythmias), kwa maana ya ugonjwa unaosababisha mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio wa kawaida.
Kuna ugonjwa wa moyo unaoitwa Atherosklerosisi (Atherosclerosis). Hali hii ni kitendo cha gmafutamafuta kuganda kwenye mishipa ya ateri. Kuganda kwa mafutamafuta huko, kunaweza kuchukua miaka mingi. Kadri miaka inavyosonga mbele, ndivyo mafutamafuta haya yanazidi kuwa magumu na kuzuia msukumo wa damu yenye oksijeni kwenye moyo.
Ikiwa mafutamafuta yataziba kabisa kwenye ateri koronari na kusababisha misuli ya moyo kukosa damu yenye oksijeni, huweza kumsababishia mtu maradhi mengine yanayoitwa Anjina (Angina), kwa maana ya maumivu makali ya kifua na Mshtuko wa Moyo (Myocardia Infarction/Heart Attack).
Anyurismu (Aneurysm) ni aina nyingine ya magonjwa ya moyo. Hiki ni kitendo cha mishipa ya ateri kuvimba kama puto kutokana na kuharibika kwa mishipa au kudhoofika kwa kuta za mishipa. Ikitokea mishipa hii ya ateri ikapasuka, husababisha damu kuvuja kwenye ubongo, hivyo kumsababishia mtu kukumbwa na Kiharusi (Stroke). Kiharusi ni ugonjwa wa kupooza unaotokana na kuingiliwa au kupungua kwa usambazaji wa damu kwenye ubongo hali inayosababisha seli za ubongo kukosa oksijeni na virutubishi.
Ugonjwa mwingine wa moyo hujulikana kwa jina la Rhumatiki ya Moyo (Rheumatic Heart Disease). Huu ni ugonjwa unasababisha kupungua utendaji kazi wa moyo kutokana na moyo kuwa na vivimbe tangu mtoto anapozaliwa (Congenital Heart Diseases), na mara nyingi huweza kusababisha vifo wakati wa utotoni.
Peripheral Vascular Disease ni ugonjwa mwingine wa moyo kwenye mishipa ya damu. Ugonjwa huu hutokea kwenye mfumo wa usambazaji wa damu nje ya ubongo na moyo. Mara nyingi, ugonjwa huu huwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea, hasa wavutaji wa sigara na wenye kisukari.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), magonjwa yasiyoambukiza kama yalivyo magonjwa ya moyo, kila mwaka huuwa watu milioni 38 duniani. Vifo vingi kati ya hivyo, hutokana na magonjwa ya moyo. Inakadiriwa kwamba watu takriban milioni 17.5 hufariki dunia kila mwaka kwa magonjwa hayo ya moyo, ikifuatiwa na magonjwa ya Saratani yanayouwa watu takriban milioni 8.2 kwa mwaka, wakati magonjwa ya njia ya hewa yanauwa watu milioni nne na Kisukari watu milioni 1.5 kila mwaka.
Kwa upande wa Tanzania, takwimu kutoka Chama cha Madaktari wa Watoto nchini (PAT), zinaonyesha kwamba takriban watoto 13, 600 huzaliwa kila mwaka wakiwa na magonjwa aina mbalimbali ya moyo, huku watoto takriban 3, 400 kati yao, wakihitaji kupatiwa matibabu kwa kufanyiwa upasuaji.
Ni nini chanzo cha magonjwa ya moyo?
Kutozingatia kanuni za ulaji bora, ni moja ya mambo yanayoongeza uwezekano wa mtu kupata magonjwa ya moyo. Kwa mfano, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, vyakula vyenye sukari nyingi, chumvi nyingi na lehemu nyingi, huku ulaji wa mbogamboga na matunda ukiwa ni wa kiwango cha chini, huongeza uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo.
Aidha, hali ya kuwa na uzito uliozidi kiasi au kuwa na unene uliopitiliza pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo mara kwa mara, huchochea pia uwezekano wa magonjwa ya moyo.
Wakati mwingine magonjwa ya moyo huweza kutokana na historia ya ugonjwa huo katika familia. Umri unapozidi miaka 50 kuna uwezekano pia wa kupatwa na magonjwa haya ya moyo, huku wanaume wakiwa kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili mapema zaidi ikilinganishwa na wanawake.
Tafiti mbalimbali ambazo FikraPevu inazo zinaonyesha kuwa magonjwa ya moyo huanza kumwandama mtu pale mambo fulani yanaposababisha sehemu ya ndani ya kuta za mishipa ya damu kuharibiwa. Mambo hayo fulani, ni pamoja na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha aina fulani za mafuta na lehemu katika damu. Hali hiyo inapompata mtu, mishipa ndani ya moyo huweza kufungamana kwa mafuta. hivyo kuleta Mshtuko wa Moyo (Heart Attack) au Kupooza, kwa maana ya Kiharusi (Stroke).
Aidha, ongezeko la lehemu huongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Kiujumla, wingi wa lehemu unakadiriwa kusababisha vifo vya watu takriban milioni 2.6 duniani kila mwaka. Kuwepo kwa sukari nyingi katika damu, husababisha ugonjwa wa Kisukari, ambao unamweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa Moyo au Kupooza/Kiharusi mara mbili zaidi ya asiye na Kisukari.
Aidha, kuwa na sukari nyingi kwenye damu kwa muda mrefu, husababisha kuganda kwa mafutamafuta kwenye mirija ya damu. Kuganda huku kunaweza sababisha kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye mishipa.
Shinikizo Kubwa la Damu, maana yake ni kwamba moyo unalazimika kusukuma damu kwa nguvu ili kutosheleza mahitaji ya mwili. Kuulazimisha moyo kufanya kazi kuliko kawaida yake, kunasababisha moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure).
Uvutaji wa sigara au utumiaji wa tumbaku kwa kutafuna au kunusa (ugoro), husababisha pia sehemu ya ndani ya kuta za mishipa ya damu kuharibiwa, hivyo kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo. Kemikali zinazopatikana kwenye tumbaku, huweza kuharibu seli za damu. Uharibifu huo wa seli, huingilia muundo na utendaji mzuri wa mishipa ya damu. Aidha, kuharibika kwa mishipa ya damu, kunachochea mafuta kuganda kwenye mishipa ya damu (Atheroskerosisi).
Unywaji pombe kupita kiasi na utumiaji wa dawa za kulevya ni hatari tena kwa hili. Unywaji pombe mara kwa mara huongeza uzito wa mwili, hali inayoweza kusababisha Shinikizo la Damu kupanda. Aidha, pombe na dawa za kulevya hudhoofisha misuli ya moyo na mishipa ya damu. Misuli na mishipa ya damu ya moyo ikishadhoofika, huweza kusababisha moyo kutofanya kazi katika ubora wake (Heart Failure).
Lakini pia, ikitokea mishipa ya damu ikaharibiwa, mafuta mwilini hujikusanya katika sehemu ya mishipa iliyoharibiwa, hivyo kutengeneza utando wa mafuta (plaque). Kadri muda unavyoendelea ndivyo mafuta haya yanavyozidi kujijenga katika sehemu hiyo hadi kufanya mishipa hiyo kuwa myembamba, hivyo kupunguza kiasi cha damu kinachobeba hewa ya oksijeni na virutubishi kwenda kwenye misuli ya moyo.
Kitendo hicho kitaalamu, huitwa Atherosklerosisi, ikimaanisha kukakamaa kwa mishipa ya ateri kutokana na mkusanyiko wa mafutamafuta ndani ya ateri. Hatimaye sehemu hiyo ikipasuka, sehemu ya seli za damu zinazoitwa pleteleti za damu (chembe ndogo mviringo ambazo zinahusika na kuganda kwa damu) ambazo husaidia mwili kuponya kidonda, hujigandisha kwenye mpasuko, hivyo kuanza kujikusanya.
Hali hii huongeza mkusanyiko, hivyo kuendelea kufanya mishipa hiyo kuwa myembamba zaidi, hivyo kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) na mtu kupata ugonjwa wa Mshtuko wa Moyo (Heart Attack).
Mkusanyiko wa mafuta na pleteleti za damu wakati mwingine, huweza kumeguka katika mfumo wa mabonge na kusafiri kwenda kuziba mishipa midogo ya damu kichwani. Hali hii ikitokea, mtu hupata Kiharusi (Stroke/Cerebrovascular Accident).
Dalili kuu za magonjwa ya moyo
Kinachosikitisha hadi sasa katika tasnia ya magonjwa ya moyo, ni kwamba mtu anaweza asione dalili zozote za moja kwa moja za magonjwa ya moyo, hadi wakati mishipa ya damu ya moyo inapokuwa imeziba kabisa au kushindwa kuruhusu damu kwa kasi na kiwango kinachotakiwa.
Mara nyingi, hakuna dalili inayojitokeza moja kwa moya kwa wagonjwa wa aina hii, hadi pale moyo wenyewe unaposhindwa kufanya kazi ghafla (Heart Attack) au mtu anapopata Kiharusi (Stroke). Zaidi ya maelezo hayo ya wataalam wa magonjwa ya moyo, dalili zinapojitokeza mapema huweza kutofautiana kutegemea na aina ya ugonjwa wa moyo, ingawa dalili hizo nazo hazijitokezi mapema kama ilivyo kwa magonjwa mengine.
Hata hivyo, dalili kuu za magonjwa ya moyo ni pamoja na maumivu ya kifua (Hii ni dalili kuu ya ugonjwa wa moyo); moyo kwenda mbio na kumfanya mtu akose pumzi au kushindwa kupumua; kuvimba miguu, tumbo na mishipa ya shingoni kujitokeza nje; maumivu ya mgongo, mabega, shingo na taya; tumbo kujaa, kichefuchefu, na kutapika; kukosa usingizi; kupoteza fahamu na kikohozi kisichokwisha.
Kilicho muhimu kutambua hapa ni kwamba hadi dalili hizo zijitokeze wazi, ni kwamba mtu huyo amekuwa akiishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu. Kwa hiyo, njia bora ya kugundua mapema dalili ya ugonjwa wa moyo ni kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.
Inashauriwa mtu kuwa na ratiba maalum ya kumuona daktari angalau mara moja kila mwaka ili kuweza kuchunguza afya ya moyo wako na mwili kiujumla. Endapo mtu atahisi maumivu ya aina yoyote kifuani, hasa baada ya kufanya mazoezi, ni muhimu kuonana na daktari haraka
 Tabibu Rabson Luhamba
 TEL.NO 0756870797/0757408469

TIBA SAHIHI YA UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA IMEPATIKANA!!!


HABARI NJEMA UGONJWA WA BAWASIRI UNAOWATESA WENGI SASA UMEPATA TIBA YA UHAKIKA
~watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba

BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA (HEMORRHOIDS)
~ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani au nnje ya haja kubwa wakati mwingine mishipa hiyo inaweza kupasuka /kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kinyama au uvimbe
~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita hemorrhoids ilhali katika lugha ya kingereza unajulikana kama piles,
~tatizo hili huwaathiri zaidi watu wazima kuliko watoto na makadirio kuwa karibia 50%ya watu wote wako hatarini kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50

AINA ZA BAWASIRI
{1}BAWASIRI YA NDANI
~hii hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa na huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
Aina hii ya bawasiri imegawanyika katika madaraja manne
@DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pake pa kawaida.
@DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya kujisaidia
@DARAJA LA TATU ~hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe
@DARAJA LA NNE ~hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
[2}BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

CHANZO CHA TATIZO LA BAWASIRI
~Ugonjwa huu wa bawasiri mpaka sasa chanzo chake hasa hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo na hukuweka katika hatari ya kupata tatizo hili
~KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
~TATIZO SUGU LA KUHARISHA
~UJAUZITO
~UZITO MKUBWA
~MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
~KUPATA KINYESI KIGUMU KWA MUDA MREFU
~ DALILI ZA BAWASIRI
👉kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa
👉kujitokeza kwa kinyama eneo la haja kubwa
👉kutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa
👉kupata kinyesi chenye damu
👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA WA BAWASIRI
~ matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri, mara nyingi wagonjwa wa bawasiri hupatiwa tiba ya kukatwa kinyama na kushauriwa kuendelea na tiba ya vyakula Lakini tiba huwa haina matokeo mazuri kwasababu baada ya Muda tatizo hujirudia kutokana na kwamba hawajatibu chanzo cha tatizo hivyo tiba nzuri ya bawasiri ni kutumia dawa itakayotibu chanzo cha tatizo huku ukiendelea na tiba ya chakula, MFANO MZURI WA DAWA NI ALO SNACA NA ANION hizo zinatibu na kuondoa tatizo moja kwa moja hivyo ni vizuri kutumia dawa hizo ili kumaliza tatizo pamoja na hayo ni vyema ukazingatia mambo yafuatayo ili KUEPUKANA na ugonjwa wa bawasiri
👉ZINGATIA KANUNI YA CHAKULA BORA KWA KUPENDELEA KULA MBOGAMBOGA        ZA MAJANI, MATUNDA NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GLASI SITA HADI 12 KWA SIKU
👉EPUKA KUTUMIA MUDA MREFU CHOONI

MADHARA YA BAWASIRI
~Ugonjwa wa bawasiri una madhara makubwa iwapo hautapatiwa tiba ya uhakika haya ni baadhi ya madhara ya bawasiri
👉KUPATA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
👉KUPATA TATIZO LA KUSHINDWA KUHIMILI KINYESI
👉HUPUNGUZA MORAL YA KUFANYA KAZI KUTOKANA NA MAUMIVU
👉HUATHIRI KISAIKOLOJIA
👉MWANAMKE HUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

NOTED :NDUGU RAFIKI KAMA UNA TATIZO HILI AU NDUGU YAKO ANA TATIZO HILI WASILIANA NAMI 0756870797 KWA USHAURI WA MATIBABU ZAIDI

matatizo Ya Uzazi

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI
KWA WANAWAKE


Tatizo la kuziba kwa mirija ya mayai ya uzazi au mirija ya kupitishia mayai ya mwanamke ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa mwanamke ambapo mwanamke anakosa uwezo wa kuzaa.
 
Mirija inapoziba yai linashindwa kukutana na mbegu ya mwanaume na kutungisha mimba.

 
Kitaalamu mirija ya mayai au ‘fallopian tubes’ pia huitwa ‘Oviducts’ au uterine tubes’ au Salpinges’.

 
Matatizo ya ugumba kwa mwanamke yana vyanzo vingi lakini kuziba kwa mirija ni tatizo kubwa ambalo huathiri wanawake wengi wenye tatizo hili. Katika makala yaliyopita tuliona uchunguzi wa kuthibitisha tatizo hili.

 
Kuziba kwa mirija ya uzazi ya mwanamke ni tatizo kubwa na ndiyo linaloongoza kusababisha ugumba kwa mwanamke ingawa hata matatizo ya vichecheo au homoni pia huchangia,wanawake wengi wanaohangaika kutafuta watoto hugundulika na tatizo la mirija kuziba.
Matatizo ya mirija ya uzazi kwa wanawake yapo wengi, mfano mirija inaweza kuvimba na kupoteza uhalisia hivyo kushindwa kutungisha mimba. Mirija inaweza kujaa usaha au maji. Tatizo hili ni kubwa lakini ukifuatilia utakuta linaweza kuzuilika.
Kuziba kwa mirija ni athari za matatizo katika kizazi.

Jinsi tatizo linavyotokea
Matatizo katika mfumo wa uzazi huanzia aidha ukeni au ndani ya kizazi. Maambukizi ya ukeni huweza kujipenyeza hadi ndani ya kizazi na kushambulia tabaka la ndani ya kizazi na mirija.
  
Maambukizi yanayoanzia ndani ya kizazi pia husambaa hadi ndani ya mirija. Mirija hushambuliwa kwa ndani na nje ya kizazi. Ikishambuliwa kwa ndani husababisha mirija kuziba na ikiwa nje ya mirija husababisha mirija kujikunja.

Matatizo ya kuziba mirija hutokea pale mwanamke anapopata maambukizi ya mara kwa mara ukeni yanayoambana na muwasho kutokwa na uchafu na usaha ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.

Maambukizi haya yasipotibiwa kikamilifu husambaa hadi katika mfuko wa uzazi na kushambulia tabaka la ndani la kizazi na kusababisha tatizo liitwalo ‘Endometriosis’ ambapo mwanamke hulalamika maumivu ya chini ya tumbo au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili nyingine tulizozielezea hapo awali.

Maambukzi toka ndani ya kizazi husambaa hadi katika mirija au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili nyingine tulizozielezea hapo chini.
Maambukizi toka ndani ya kizazi husambaa  hadi katika mirija ambapo hushambulia mrija mmoja au yote miwili, hapo mgonjwa huendelea  kulalamika maumivu chini ya tumbo au yanaweza kuwa yamekwisha lakini maambukizi yaliyojipenyeza huweza kutafuna mirija na kuziba au kusababisha usaha, maji na kuvimba.
Maambukizi yanaweza kutokea nje ya kizazi na mirija na kusababisha mirija ijikunje na kuziba kabisa hali iitwayo ‘Adhesions’. Maambukizi yanayoanzia ndani ya kizazi chanzo chake ni utoaji wa mimba au mimba kuharibika.
Mirija inaweza kuziba ambapo itakatwa kwa lengo la kufunga uzazi, inaweza kuziba kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye kizazi.
Upasuaji wa mirija kwa lengo la kuzibua pia inaweza kuongeza tatizo kwani itatengeneza makovu ambapo mirija itaziba tena. Maambukizi ya muda mrefu ukeni au katika mfumo wa uzazi huathiri mirija ya uzazi.


Dalili za kuziba mirija
Mwanamke anayedhaniwa mirija imeziba anakuwa na historia ya kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mafanikio.Historia hiyo inahusiana na kuwa na historia ya kusumbuliwa na maumivu ya chini ya tumbo kwa muda mrefu iwe yameshatibiwa au la.
Wengine wanakuwa na historia ya kuzaa angalau mtoto mmoja au zaidi lakini anatafuta mwingine anashindwa kupata. Mwingine ana historia ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo

Wengi wenye tatizo hili wana historia ya kuharibikiwa na mimba au kutoa mimba hata moja tu inaweza kukuzibia mirija yako ya uzazi. Endapo mrija mmoja utazibika kabisa basi unaweza kuzaa hata watoto zaidi ya mmoja kwa kutumia mrija mmoja.

Nini cha kufanya?
Tatizo la kuziba kwa mirija linathibitishwa hospitali ambapo kipimo kinachoitwa ‘HGS’ hufanyika ili kuthibitisha. Kipimo hiki ndicho kinachoonyesha kwa usahihi jinsi mrija ulivyoziba, upo uzibaji ambao mrija baadaye unaweza kurekebishwa na mwanamke akapata  ujauzito. Picha nzuri ndiyo itakayomuelekeza daktari jinsi ya kuurekebisha mrija.
Mrija ukiziba nusu yaani ukiachia nafasi kidogo kama hautarekebishwa basi kuna hatari ya kupata mimba na ikabakia kukua kwenye mrija na hatima yake ni mrija kupasuka na kuupoteza.
Muone Tabibu wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika Clinic  kwa uchunguzi na tiba utafanikiwa.
Imeandaliwa na Dr.Luhamba